Utunzi wa kielimu

معلومات المواد باللغة العربية

Audios

Idadi ya Vipengele: 248

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia umuhimu wa elimu ya dini na kubainisha haki ya mtoto katika kumsomesha elimu ya dini,na majukumu ya wazazi kwa watoto,khatari ya kusoma katika mashule ya kikafiri.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia umuhimu wa hisba katika uislam,maana yake na uwajibu wa hisba na mfano wa hisba katika wakati wa mtume.

  • Kiswahili

    MP3

  • Kiswahili

    MP3

    Commanding Beneficence And Forbiding Maleficence

  • Kiswahili

    MP3

    Maana ya Aibu pila ameeleza kua Allah anazijua siri zetu, kisha ameeleza udhaifu wa mwanadamu na tabia za watu katika kusema aibu za wenzao, na tiba ya maradhi ya kutangaza aibu za watu.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inaelezea nafasi ya nia katika ibada, ameeleza maana ya nia na mahala pake katika ibada na jinsi ya uweka nia katika ibada.

  • Kiswahili

    MP3

    1. Mada hii inaelezea: Maana ya kusengenya (Umbeya) na kwamba ni katika madhambi makubwa, kisha amebainisha sifa za watu wenye umbeya, na kwamba nimtu washari, na ataadhibiwa katika kaburi lake. 2. Mada hii inaelezea hatuwa za kufanya katika kutibu maradhi ya Umbeya, na katika hatuwa hizo ni kuthibitisha habari unazo zipata, kisha akaeleza kuwa waganga wa kienyeji(Washirikina) na wachawi nikatika wanao ongoza kwa kusengenyaji(Umbeya).

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia Maada ya pombe na hukumu ya kutumia na kuuza pombe, kisha amebainisha kuwa madawa ya kulevya ni katika yana hukumu ya pombe, na ameelezea madhara ya madawa ya kulevya kiafya kidini na kijamii na kwamba pombe ni mama wa Machafu.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia sababu za kupata mali, miongoni mwa sababu hizo: Ni Uchamungu, na ukweli katika maneno na vitendo na katika niya yake, hiyo nisababu ya kutengamaa mambo yote.

  • Kiswahili

    MP3

    1. Mada hii inazungumzia Umuhimu wa kuwa mchamungu na hasara za kukosa uchamungu kisha akaelezea kuwa Mwaka mpya nimwaka wa kuihesabu Nafsi. 2. Mada hii imezungumzia ufupi wa umri wa mwanadamu, nakwamba ameumbwa kutokana na masiku, kisha akabainisha kuwa katika kuihesabu nafsi nikujuwa mema aliyo yafanya, na kwamba kuikaguwa nafsi nikatika alama ya Uchamungu. 3. Mada hii inazungumzia miongoni mwa kuihesabu nafsi ni kuihesab nafsi na kujuwa chanzo cha uovu wake, na kwanini inapata uzito wa kuswali! Kisha amezungumzia umuhimu wa kujuwa uhalali na uharamu wa vyakula vyetu, na kwamba mtu asie swali nikafiri. 4. Mada inazungumzia Miongoni mwa kuihesabu nafsi nikutekeleza ibada ya swala, na familia yote, na kwamba swala ndio funguo za rizki, kisha ameeleza hali ya watu na swala zao pindi wanapo safiri zao, pia ameleza umuhimu wa kuhesabu mali ili kuzitolea zaka.

  • Kiswahili

    MP3

    1. Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa Uchamungu, na maana ya khutbatu Alhaja, kisha akabainisha swala ya khusufu na Malengo ya khusufu. 2. Mada hii inazungumzia: Fursa ya kuyafikiwa na masiku bora duniani, kisha ametaja miezi mitukufu, na akaeleza ubora wa masiku hayo, na ubora wa siku ya Arafa. 3. Mada hii inazungumzia: umuhimu wa kufunga siku ya arafa, na mambo anayo takiwa afanye katika masiku kumi ya mfungo tatu. 4. Mada hii inazungumzia:miongoni mwa matendo mema katika masiku kumi ya mfungo tatu, na amebainisha ubora wa kutowa salam, Kuunga udugu na kuwafanyia wema wazazi, na kuchunga haki za mume na mke.

  • Kiswahili

    MP3

    1. Mada hii inazungumzia khutba ya mkosi na sababu ya kuitwa hivyo pia amezungumzia vitisho vya siku ya Qiyama. 2. Mada hii inakamilisha mada iliyo pita imeelezea hali za watu wamotoni na vyakula vyao na nguo zao, pia mezungumzia maneno ya shetani atakayo zungumza motoni.

  • Kiswahili

    MP3

    Silsila ya mada za sauti za Tarjama ya Quran tukufu kwa lugha ya kiswahili inayo itwa "Al Muntakhab Fi Tafsir Al Qur’an" iliyo fanywa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani tafsiri hii inasifika kwa ufasaha wa lugha, masahafu huu umekusanya sauti ya msomaji wa Quraan, na sauti ya anaesoma tarjama ya kiswahili.

  • Kiswahili

    MP3

    1- Mada hii inazungumzia: Sifa za Ghurabaa waliotajwa na Mtume (s.a.w), kwamba ni wale wanaotengeneza pindi watu wanapo haribu, pia imezunguzia Ghurabaa ni wale wanao shikamana na Manhaji ya Mtume (s.a.w). 2- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sifa za Ghurabaa ni kushikamana na Sunna na kuthibiti katika haki na kujiepusha na mambo ya batili, bid’a na uzushi, pia imezungumzia umuhimu wa kusoma na kuujua uislam.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kuitekeleza nguzo ya Hajj, wanaopaswa kuitekeleza na namna ya kuitekeleza, pia imezungumzia miezi maalum ya Hajj kama ilivyotajwa katika Qur’an tukufu ambayo ni Shawwal, Dhul-Qaada na Dhul-Hijja

  • Kiswahili

    MP3

    1- Mada hii inazungumzia: Nafasi ya vijana katika uislam, na neema ya ujana, na kila kijana ataulizwa siku ya qiyama, pia amezungumzia uwajibu wa vijana kuutumia ujana wao katika kufanya ibada, kama kusimamisha Swala, Funga na Hijja, ili kupata radhi za Allah. 2- Mada hii inazungumzia: Vijana ni hazina kubwa katika uislam tangu zamani, nakwamba vijana ndio wenye uwezo wa kuvumilia mashaka na misukosuko, pia imezungumzia umuhimu wa vijana kujipamba na tabia njema.

  • Kiswahili

    MP3

    Mhadhiri : Arafat Magmoud Kurejea : Yasini Twaha Hassani

    1- Mada hii inazungumzia: Neema za nyumba na faidazake, nakwamba nyumba niukamilifu wa neema za Allah kwa waja wake, pia imezungumzia baadhi ya faida za nyumba kama vile makazi, stara, kulala, ibada ya swala na ibada ya ndoa. 2- Mada hii inazungumzia: Nyumba ni sehem ya kumstiri mwanamke na kumlinda na swala iliyo bora kwa mwanamke ni nyumbani, na wanawake wema ni wale wenye kutulia majumbani mwao, pia imezungumzia umuhimu wa kuwafundisha dini na adabu wake na watoto katika majumba. 3- Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kuwafundisha wanawake na watoto mambo ya Sunna na mavazi ya stara ili kuepuka masuuliya siku ya Qiyama, pia imezungumzia ubora wa kulazimiana na nyumba na kutenga muda kwa ajili ya kumtaja Allah ili kuepukana na fitna. 4- Mada hii inazungumzia: Nyumba ni nyenzo kubwa ya kujenga jamii ya kiislam na kutoa wanachuoni pamoja na wanawake wema, pia imezungumzia umuhimu wa mzazi kuwaombea dua ya kheri wanae.

  • Kiswahili

    MP3

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    1- Mada hii inazungumzia: Maana ya Hijja kilugha na kisheria, na ni nguzo katika nguzo tano za uislam, pia imebainisha kwamba Hijja ni fardhi inatekelezwa mara moja katika umri. 2- Mada hii inazungumzia: Umuhimu kwa mwenye kuhiji kuwa na nia thabiti pamoja na kujikurubisha kwa Allah, pia imezungumzia mambo ya kujifunza katika ibada ya Hijja na tahadhari ya kuiga uzushi. 3- Mada hii inazungumzia: Hijja na Umra na fadhila zake pamoja na alama za mwenye kufanya Hijja ya kweli, pia imezungumzia kwamba Hijja ni fardhi kwa waislam wote wanaume na wanawake. 4- Mada hii inazungumzia: Aina za maandalizi ya Hijja na imefafanua kuhusu Hijja ya mtoto mdogo, pia imezungumzia umuhimu wa kuchunga utaratibu na makatazo baada ya Ihram. 5- Mada hii inazungumzia: Namna Mtume (s.a.w) alivyoruhusu kumuhijia mzazi asiyejiweza kutokana na uzee au ugonjwa, na kwamba inafaa mwanaume kumuhijia mwanamke na mwanamke kumuhijia mwanaume, pia mada hii ina maswali na majibu.

  • Kiswahili

    MP3

    1- Mada hii inazungumzia: Hijja ni wajibu kwa Muislam ambaye ni baleghe mwenye akili mwenye uwezo tena mukalafu aliye huru, pia imezungumzia hasara ya mtu mwenye uwezo kisha akafa bila ya kuhiji. 2- Mada hii inazungumzia: Uzembe unaofanywa na baadhi ya waislam wenye uwezo katika kuitekeleza Hija na kwamba ni hasara kubwa kwa watu kama hao, pia imezungumzia kuwa hija ni mara moja tu katika umri

  • Kiswahili

    MP3

    1- Mada hii inazunguzia: Umuhimu na nafasi ya Hijja katika Uislam na kwamba Hijja ni wajibu na inatekelezwa kwa ajili ya Allah peke yake, pia imezungumzia ruhusa aliyoitoa Mtume (s.a.w) ya kumfanyia Mzazi Hijja. 2- Mada hii inazunguzia: Umuhimu wa hija na umuhimu wa kuwafanyia hija wazazi walio fariki, na kuwafanyia wema wazazi kwa kuwawekea waqfu, na amezungumzia nyakati za hijja pia amebainisha ubora wa kuhiji ukiwa kijana.