104 - Surat Al-Humazah ()

|

(1) Ole wake kila safihi, msengenyaji!

(2) Aliyekusanya mali na kuyahesabu.

(3) Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele!

(4) Hasha! Atavurumishwa katika Hut'ama.

(5) Na nani atakujuvya ni nini Hut'ama?

(6) Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa.

(7) Ambao unapanda nyoyoni.

(8) Hakika huo utafungiwa nao.

(9) Kwenye nguzo zilizonyooshwa.