99 - Surat Az-Zalzalah ()

|

(1) Itakapotetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!

(2) Na itakapotoa ardhi mizigo yake!

(3) Na mtu akasema: Ina nini?

(4) Siku hiyo itahadithia habari zake.

(5) Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!

(6) Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!

(7) Basi anayetenda chembe ya wema, atauona!

(8) Na anayetenda chembe ya uovu atauona!