113 - Surat Al-Falaq ()
|
(1) Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko.
(2) Kutokana na shari ya alivyoviumba.
(3) Na kutokana na shari ya giza la usiku liingiapo.
(4) Na kutokana na shari ya wanaopulizia mafundoni.
(5) Na kutokana na shari ya hasidi anapohusudu.