114 - Surat An-Nas ()

|

(1) Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanadamu.

(2) Mfalme wa wanadamu.

(3) Mungu wa wanadamu.

(4) Kutokana na shari ya Shetani mtia wasiwasi, ajifichaye mno (Al-Khannaas).

(5) Anayetia wasiwasi katika vifua vya watu.

(6) Kutokana na majini na wanadamu.