(1) Kwa walivyozoea Maqureshi.
(2) Kuzoea kwao safari za siku za baridi na siku za joto.
(3) Basi na wamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii.
(4) Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na hofu.