111 - Surat Al-Masad ()
|
(1) Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia.
(2) Haitamfaa mali yake, wala alivyovichuma.
(3) Atauingia Moto wenye mwako mkali.
(4) Na mkewe, mchukuzi mkubwa wa kuni.
(5) Shingoni mwake iko kamba iliyosokotwa sawasawa.